cover

SIRI YA HUDUMA YA UIMBAJI

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church • 2022-12-19
ScripturesZab 119:164-165

Mambo 7 baba amefundisha kuhusu Huduma ya uimbaji. Baba alisisitiza kuwa Kuna hatua hatutapiga kiroho au kimwili pasipokujua Siri iliyojificha ktk uimbaji. Kwa ufupi sana nitasema, 1.Mungu huketi mahali pa sifa.Ziko shughuli nyingi sana mbinguni mfano hukumu, karama ya mwanakondoo lakini shughuli kuu ni uimbaji. 2.Huduma ya sifa inaweza kukugeuza ukawa chochote.Ziko Huduma kuu mbili Duniani ambazo ni hatarishi.Huduma ya utoaji na uimbaji.Mtoaji wa kwanza Habili aliuawa.Uimbaji ulimgeuza Lucifer malaika na amekuwa shetani mpaka hivi Leo. 3.Huduma ya sifa hulegeza na kufungua vifungo..Matendo 16:16-29.Wakati mwingine baba alisema akimaliza kuhubiri injili huimba sifa.Paulo na Sila waliimba gerezani tetemeko likatokea na milango ya gereza ikafunguka. 4.Huduma ya Sifa ni ufunguo wa utetezi wa Mungu juu ya maadui.2Nyakati 20:1- 4.Yehoshefati alitishwa na maadui Mungu akampa maelekezo kupitia nabii kutanguliza waimba sifa in the battle field.Maadui wakageukiana Kwa upanga.Zaburi za Daudi pia ni nyimbo za sifa. 5.Huduma ya sifa hufungua malango ya uzao.Isaya 54:1 Imba wewe uliyetasa, Watoto wako wanakuja.Kwa sifa unaweza kuzaa mafanikio ktk Kila eneo la maisha.Nyimbo za sifa zinaweza kuzaa biashara,kazi,ndoa,elimu nk. 6.Huduma ya sifa huinua mioyo Tena.Mioyo inaweza kuhuishwa Tena Kwa sifa.Yakobo 5:13 7.Huduma ya sifa hukuandaa kwenda ktk wito Mkuu.Haijalishi unapitia Hali Gani, sifa itakupeleka kwenye kusudi.Mathayo 26:30' walipokwisha kuimba wakaenda milima ya mizeituni.

Comments

Tatu Kazimoto — 2026-01-20 09:47
Nimebarikiwa

Please login to comment.