Habari Njema ya Bwana Yesu Kristo
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; — Tito 2:11 —
Haleluya! Bwana Yesu asifiwe sana rafiki zangu. Yesu anakupenda sana na anatamani umgeukie na kumwamini yeye kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Neema hiyo iliyofunuliwa ni Yesu Kristo, naye yu karibu kurudi, ndugu yangu. Hebu chunguza maisha yako: akisema sasa anarudi, je, utaketi naye mawinguni?
Ndugu, jehanamu ipo na mbingu ipo. Neno la Mungu linasema katika Matendo ya Mitume 3:19: “Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.” Siku ya mwisho ipo na inatisha. Ndugu yangu, badilisha tabia yako na mwenendo wako kabla hazijaja siku za hatari. Maana kumbuka kiburi cha mwanadamu kina mwisho.
Ikiwa umemwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, fuatisha sala hii:
"Ee Bwana Yesu, nakiri dhambi zangu na makosa yangu yote niliyokukosea. Leo nimeamua kukupokea kuwa Bwana, Mwokozi, na Kiongozi wa maisha yangu. Ingia ndani ya maisha yangu, fanya makao yako. Amina."
Tupigie namba hizi au tuma ujumbe wa SMS/WhatsApp:
0715-402-238 au 0762-738-462
ili tuweze kuomba nawe pia.
Mtd 2:42
Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Ufunuo 12:11
"Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa"
Tovuti Yetu
Tunaeneza Injili kupitia mafundisho, maombi na mahubiri katika jina la YESU KRISTO.
“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”
— Wafilipi 4:6
Mungu akubariki sana unapotafuta uso Wake! 🙏