cover

UKOMBOZI WA NYOTA

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church •
ScripturesMathayo 2:1-12

MAMBO YA KUJUA 1. Kukosa maarifa kwa habari ya ulimwengu wa roho(kumeliingiza kanisa kwenye hasara na bado watu hawajajua wanateseka. -Somo la nyota ni somo linalohusiana na ulimwengu wa roho. 2. Ni rahisi sana kwa mtu kuotea ibada zake, lakini hakuna mchawi/mganga anayejaribu/anayeotea. Epuka sana kujaribu/kuotea maana haitatokea ukafanikiwa kwa kujaribu/kuotea. 3. Maarifa kuhusu nyota yako ni muhimu kujua kama kanisa, lakini inabidi kujua Mungu yupo kinyume na wasoma nyota. Mathayo 2:1-12 -Waganga(wanajimu) ndio waliokuwa wa kwanza kujua Yesu amezaliwa. -Nyota ya Yesu iliwaongoza wanajimu alipokuwapo Yesu(Hii ina maana; mfumo wa nyota ndio utakaomwelekeza shetani popote ulipo; nyota yako ni direction tosha kwa shetani) - Kuzaliwa kwa Yesu (nyota ya Yesu) kumlifadhaisha Herode na Yerusalem yote; Kwa nini Herode anafadhaika? Kwa sababu ya kitu alichobeba Yesu(Kadhalika na wewe, kitu ulichobeba ndani yako kinamfadhaisha shetani na mawakala zake wote.) Dad anasema, “Nyota ya mtu ni kama sumaku(magnet), inaweza kuvuta chochote.” 4. Kuna mambo kadhaa ambayo nyota ya mtu inaweza fanyiwa katika ulimwengu wa roho: i) Nyota inaweza kuzimwa. Ayubu 3:9 Nyota ya mtu ikizimwa anakutana na ugumu wa maisha, utawashauri wengine na wakafanikiwa, lakini mambo hayo hayo uliowashauri wewe ukiyafanya hufanikiwi.. ii) Nyota inaweza kuibwa au kuhamishiwa kwa mtu mwingine. -Watu wanaweza kutajiriki kupitia nyota yako. iii)Nyota ya mtu inaweza kuinamishwa. Unakuwa mtu wa kukataliwa, kuonewa, utakopeshwa na hutalipwa, unakuwa mtumwa wa watu wengine. Mwanzo 37:9 5. Watu ambao nyota zao zipo hatarini./Aina za nyota zilizo hatarini(kuibwa, kuzimwa au kuinamishwa). ➡️NYOTA ZA UTAWALA(watawala) Maana ya nyota(uwezo binafsi uliopewa na Mungu) -Endapo utazaliwa na wasoma nyota wakagundua kuwa wewe ni mtawala, tayari upo hatarini kuibiwa nyota yako.) Mfano Yesu alipozaliwa nyota yake ilionyesha ni mtawala amezaliwa. -Hapo ndio pale unajikuta unaongozwa badala ya kuwa kiongozi. Lakini kwa neema ya Mungu alioiachilia na maarifa haya kwa jina la Yesu, patakuchaa.. “Ukiniroga una hasara, maana Mungu hazuii ubaya, Mungu anazuia ramani za ubaya tangu awali.” ➡️NYOTA YA UTAJIRI(wote wenye alama ya utajiri) Ukishahisi kama una alama ya utajiri ndani yako, kuna kitu unatakiwa ukijue haraka kabla nyota hiyo haijahamishwa. ➡️MAHUSIANO NA NDOA. Hapa ndio pale watu wasio kuwa na nyota ya kuoa au kuolewa wanaiba kichawi nyota kwa watu waliopewa nyota hiyo. -Shetani anaweza iba nyota yako akaruhusu uolewe kabisa lakini na mwanaume ambaye ameibiwa nyota ya utajiri. Umeolewa, una amani lakini unakosa chakula, uzao, utajiri n.k Dad anasema, “Kila kitu katika ulimwengu wa roho ni bidhaa. Mfano damu ya Yesu(ilitununua) -Damu ya ng’ombe, kuku n.k(bidhaa hizi zinatumika katika ulimwengu wa kishetani.) ➡️ELIMU(kipawa cha masomo) There are people we call, STAR HUNTERS(wawindaji wa nyota.) Wawindaji wa nyota wanajua toka awali kwamba mtoto huyu anaweza kufika hatua fulani kielimu, wanachokifanya wanaiba nyota na kumlumbukizia magonjwa/tabia mbaya n.k Mtoto anasoma kabisa lakini akifikia kiwango fulani anaanza kuteseka na kushindwa kuendelea. Daniel 1:4(Akina Daniel walikuwa na nyota ya elimu) ➡️NYOTA YA BIASHARA Kuna watu wana mkono wa biashara na chochote wanachouza kinauzika. Shetani anaweza pia kuwawinda na kuwaibia nyota zao. NJIA ANAZOTUMIA SHETANI KUNASA/KUIBA NYOTA ZA WATU. 1. WAGANGA WA KIENYEJI/wachawi. “Wengi walipoenda kwa waganga kusafisha nyota, hapo ndipo waganga walipata fursa ya kuiba nyota zao, unafikiri wamekusafisha kumbe ndio wameiba. 2.MAWAKALA WA GIZA Shetani hutuma mawakala zake kuiba nyota za watu. Watakuja kama wenye upendo mwingi kwetu lakini ukichunguza kwa jicho la rohoni, wana Agenda maalumu na nyota yako. -“Si kila kizuri kina uzuri ndani yake na si kila kibaya kina ubaya ndani yake, ni lazima uwe na jicho la rohoni kutambua yupi mwema na yupi mbaya.” Mfano Busu la Yuda kwa Yesu. Ni kama liliashiria upendo lakini kiukweli lilibeba mauti. 3. KUDHARAU/kutokuzingatia ulimwengu wa roho. -Kuna siku baba aliwahi sema, “Kitendo cha wewe kutokuona, haimaanishi kuna mambo hayaendelei/hayatokei katika ulimwengu wa roho” Ni lazima kuwa makini sana kwa habari nzima ya ulimwengu wa roho. SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA HATA KAMA UMEOKOKA, NYOTA YAKO KUIBWA. 1. Maisha vuguvugu kiroho -Wiki moja una Yesu, wiki moja una shetani. Hueleweki uko ndani au nje, lazima nyota yako iwindwe. 2. Kutokusimama katika nafasi yako ipasavyo. Kuna nafasi ambayo Mungu amekuweka kwayo (Mtumishi wa madhabahu, mchungaji, shemasi n.k) husimami kwenye nafasi yako vizuri kuna hatari ya nyota yako kuibwa. 3. Kutokujua/kudharau ulimwengu wa roho. #Haya maarifa yamefunuliwa kwa wakati maalumu. Mungu hajataka twende 2023 hali tukiwa tumeibiwa nyota zetu, tukaanza vibaya. Mungu ametaka twende tukiwa safi ili atuinue na baraka zake zipate kukaa. Kumbuka Mungu akikubariki, anakutaka wewe. God bless you our father in spirit. Umekuwa baraka sana kwetu natamani tungeendelea kusikia zaidi kuhusu hizi habari za ndoto ili tukitoka tumetoka mazima. May God bless the Nation of Rgcm

Comments

No comments yet.

Please login to comment.