FAIDA ZA KUMUOMBEA baba YAKO wa KIROHO
ScripturesMathayo 26:36
Jina la BWANA YESU lisifiwe
Shalom baba & mama
Senior pastor
Shalom watumishi wa BWANA MUNGU Aliye Juu.
SOMO : FAIDA ZA KUMUOMBEA baba YAKO wa KIROHO
Wiki hii BWANA YESU alinipa maono namna ambavyo huduma hii BWANA YESU anaipeleka.
Kwa KWELI ni mahali pa UTUKUFU na BWANA YESU ataendelea kutukuzwa na atatukuzwa. Lakini ghafla katikati ya yale maono nikaona msukumo wa Kumuombea Mtumishi wa MUNGU.
na leo nishare tafakari hi Kwako Mtumishi mwenzangu. Unapata Muda wa Kumuombea baba yako wa Kiroho ? Kuombea Familia yake na Huduma.
Je Unajua kwamba Yeye Kiuhalisia anaihitaji maombi yetu Zaidi kuliko sisi tunavyohitaji maombi kutoka kwake ?.
Kila kiwango cha Huduma kina level ya maombi yanayohitajika. Mathayo 26:36
Inatuonyesha namna wanafunzi wa BWANA YESU walivyofika kwenye Bustan ya Eden. pale Gethsamane.
Kiwango cha Huduma na aina ya Maombi haikuhitaji tu maombi ya saa 1 au mbili. yalihitaji maombi ya mkesha. kuomba Mpaka asubuhi. Pia BWANA akawa anahuzunika na kusema " Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. " Hii ni ishara ya kuwa wanafunzi walipaswa kuelekeza maombi yao kwa BWANA YESU.
Ni Ajabu kuu BWANA YESU na yeye alihitaji maombi kutoka kwa wanafunzi wake , Je si Zaidi sana kwa baba yetu Ev. Daniel.?
Sasa tuone hasara walizopata wanafunzi kwa kushindwa kuomba kwa ajili ya baba yao wa kiroho na zinaweza kuwa faida kwetu kama tukiomba kwa ajili ya baba yetu Ev. Daniel
Kupigana vita Kiroho kunakopelekea Ushindi.
Mathayo 26:51
" Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio."
Hapa tunaona namna ambavyo majaribu yalivyotokea tenashara wakaingia mwilini. BWANA YESU alipokamatwa , Petro akatoa panga akamkata mtu sikio. Kwa Sheria za sasa PEtro angeenda Jela miaka 15 au 30 kwa kukosa la kutaka kuua ( Manslaughter case ).
Kanisa la mwanzo lilijua siri hii , Petro alipokamatwa na Herode hawakuandamana, hawakuchukua mabango yao na kuanza kupigana na Polisi wa wakati huo
bali waliingia kwa maombi na BWANA akatuma Malaika akamtoa Petro.
2. Roho ya Kuambatana na Mtumishi hadi Mwisho
Majaribu yalipotokea walikimbia wanafunzi wote. Hadi Petro akafika mahali pa kumkana BWANA. Ni rehema za BWANA tu zilimvuta tena.
Tunapoomba kwa ajili ya baba yetu , tunapewa roho ya uaminifu na roho ya uwana inayotupa neema ya kuambatana Mpaka Mwisho.
Mwisho wapendwa Tuzidi kuombeana kadri ya siku ile kuu inavyokaribia. Ahsante ROHO MTAKATIFU
Mimi mjoli wa BWANA.
Evangelist David Joshua