cover

VIWANGO VYA SHUKURANI NA SABABU YA ZASHUKURANI MBELE ZA MUNGU

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church • 2024-04-21
ScripturesLuka 17:15-19

VIWANGO VYA SHUKURANI NA SABABU YA ZASHUKURANI MBELE ZA MUNGU Na Ev, Daniely Joshuan 21st April 2024 Naomba ujue kwamba wengi wameshindwa kutembea na Mungu na kushindwa kutembea na wanadamu wenzao kwa kushindwa maombo mawili. Msamaha Kushukuru. Maneno haya mawili ndiyo msingi wa Dunia, nisamehe na Asante. Ukitaka kwenda na Mungu vizuri au na watu vizuri lazima ujifunze kusema Asante au Nisamehe. Kukosa shukurani kunamzuia Mungu kufanya kwa ukubwa ule ule alioufanya. Kuna watu Mungu anawafanyia lakini kuna wanaofanyiwa kwa ukubwa. Usipomshukuru Mungu hawezi kukufanyia kwa ukubwa ule ule aliofanya mwanzo. Usipojua kuahukuru utakuwa na baraka za jumla, namaanisha mvua inawenyeshea wote waovu na wema. Je unataka Mungu afanye kwa ukubwa? Kidole chake kimoja kinaweza kusababisha maisha yako kubadilika. Tunamuamini na kumuhubiri Mungu ambaye anaweza kumchukua mtu gerezani na kumfanya kuwa waziri mkuu. Mungu ambaye anaweza kumchukua chokoraa asiyefaa na kumfanya kuwa malkia. Mtumishi mmoja alikuwa anapitia mambo magumu na anateseka huku na kule. Wakamletea mtu mwenye kansa na alikuwa hana eneo la huduma. Wakampelekea mtu mwenye kansa na bajaji na alikuwa amenyolewa na alikuwa tajiri. Alipoenda kupima akakuta hana kansa akarejea kwa mtumishi. Walipomrudisha akaenda huku amechangamka kwenye nyumba ambayo haikuwa njema ya mtumishi. Yule Dada alibadilisha maisha ya mtumishi kabisa, alimpa Gari pamoja na nyumba. Bwana aliniambia niongee na wewe kwamba usiposhukuru kwa yale aliyotenda kwa ukubwa wa alichokufanyia, uwe na uhakika Mungu hatajifunu kwako. Hiki ni kilio cha watu wengi ambao wanalia na watumishi wengine ambao hwwakujua namna ya kumshukuru Mungu. Kuna vitu ukiona unasema hii ni mkono wa Mungu. Unakumbuka habari ya wakoma kumi mbao walienda kwanYesu wakiomba uponyaji. Aliwaponya kumi lakini akarejea mmoja kushukuru. Luka 17:15-19 [15]Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; [16]akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria [17]Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? [18]Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? [19]Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa. Wengi wasiposhukuru baada ya muda wanakuta tatizo limerejea pale pale. Hili uweze kuwa na shukurani mbele za Mungu kuna viwango sita vya shukurani. Kiwango cha Kwanza Maneno yatokayo moyoni Unaweza kumuambia Asante lakini haijatoka moyoni ni Asante ya kupumbaza. Haujawahi kusikia mtu akisema acha nimuambie Asante tu asije kujisikia vibaya. Asante ya kupumbaza. Ndiyo maana Yesu anasema watu hawa wananiabudu kwa midomo yao tu lakini mioyo yao iko mbali nami. Kiwango cha kwanza cha kutoa shukurani lazima itoke moyoni. Zaburi 119:7 Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako Lazima asante itoke moyoni si kwasababu unataka kumfurahisha yeyote lazima itoke moyoni mwako. Nimejifunza na kugundua watu wenye mioyo minyoofu lazima wamuone Mungu. Hakuna namna ambavyo moyo ukawa na hila na umuone Mungu. Ukitaka kujifunza kuwa Mkristo halisi hakikisha unaufundisha moyo wako. Vitu vinne fundisha moyo wako 1️⃣ Fundisha moyo wako kuwa kimya 2️⃣ Fundisha moyo wako kusikiliza. 3️⃣ Fundisha moyo wako kujifurahia na kufurahia wengine. 4️⃣ Fundisha moyo wako kunyenyekea. Kiwango cha Pili Shukurani kwa maisha yako. Namna unavyoishi ni ishara ya shukurani. Mungu ikikuinua namna unavyoishi ndiyo shukurani yako. Mungu anamuinua mtu namna ya shukurani anaenda kuoa mke wa pili. Haujawahi kuona watu wakisema hii ndo shukurani yake nimemsomesha analala na mme au mke wangu. Hivyi aina ya maisha unayoishi ni shukurani, je? Maisha unayoishi yanampa Mungu shukurani. Hivyo kiwango kingine cha Asante ni aina ya maisha unayoishi. Hichi ndicho kilifanyika kwa wana wa Israeli maisha yao hayakuhakisi kile ambacho Mungu aliwafanyia. Mfumo wa maisha ya mtu yanaonyesha ishara ya shukurani. Baada ya baraka na kujua maisha yako yanaakisi nini? Wengi Mungu alipowainua na kuwabariki waliacha kanisa, waliacha huduma waliokuwa wanafanya. Wengi walipobarikiwa wakawa na viburi maana yake hiyo ndiyo Asante yao. Kama kwenye maisha yako kuna mtu ambaye alikusaidia na ukapita mahali muheshimu hata kama kuna baya ambalo amefanya. Jambo la Tatu Shukurani kwa njia ya sadaka. Hii ndiyo watu wengi wanajua, kutoa sadska ya shukurani. Mara nyingine hata hizo sadaka zenyewe hazikuw sawa sawa. Ndiyo maana unakuta mtu anataka kutoa na anaona anachotaka kutoa hakitoshi. Sasa hicho kitendo tu kinaonyesha tayari imekataliwa, kama moyo wako haujatoa basi Mungu hajaipokea hiyo sadaka. Jambo la Tano _* Utoaji kupitia utoaji*_ Hakuna baraka za jumla kwa utoaji wa sadaka. Kwa mfano ukitaka baraka ya ulinzi wa kiuchumi sadaka inayohusika hapo ni fungu la kumi. Ukitaka kukopesha Mungu wape masikini. 2 Mambo ya Nyakati 29:31 Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa. Yeremia 17:26 Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, na milima, na upande wa Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA Kiwango cha Sita Shukurani kwa njia ya Nyimbo Hii ilikuwa shukurani ambayo Daudi alikuwa akifanya. Kuna aina nyingi za nyimbo, za vita, nyimbo za maombolezo lakini kuna nyimbo za shukurani. Zaburi 71:22 Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli. Shukurani mbele za watu wote Mshukuru Mungu mbele za wafanya biashara wenzako. Usisahau kumtambulisha Mungu wako, maelezo madogo sana lakini yanayomshukuru Mungu wako. Kuna watu wana vyeo ambao hawawezi hata kumsemeha Mungu wao, wakiwa kwenye kiti fulani utasikia tuendelee na kile kimetuleta hapa. Sikiliza wewe si wakwanza kukaa kwenye nafasi hiyo na wala hauko kwenye nafasi hiyo kwa bahati mbaya, Mungu amekuweka hapo. Zaburi 35:18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi. Kuna mahali unaangalia ushuhuda na unaona lazima niseme katika kusanyiko si swala la kujifungia ndani. Zaburi 18:49; 57:9 Shukurani ya Milele Unamshukuru Mungu hapa duniani na ukifika mbinguni ukazidi kushukuru. Zaburi 30:12 Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele. Daudi alipokuwa anasema namna hii hakuwa anasema kwasababu ya kusema tu. Daudi alikuwa na nafasi mbele za Mungu wakati akiwa hai na alikuwa na nafasi baada ya kufa. Siku ya kuingia mbinguni ndipo utajua namna ya kumshukuru Mungu kwa nafasi ya kuokoka.

Comments

No comments yet.

Please login to comment.