cover

UJUMBE WA MUNGU KWA KANISA KUHUSU KIBURI

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church • 2023-11-28
ScripturesMithali4:23

Shalom Baba,Kuhani na Nabii wetu!Asante kwa ibada hii,huwa unatuambia "kukamilishwa siyo issue ya siku moja bali ni mchakato"🙏🏿🙌🏿 UTANGULIZI:UJUMBE WA MUNGU KWA KANISA KUHUSU KIBURI ✍🏻Somo la killing the pride lipo youtube Baba alishafundisha(tulirudie/kulifatilia) ✍🏻Kanisa la nyakati za mwisho tunapaswa kujifunza sana katika eneo la moyo;maana kanisa litakalokuwa imara limefungamanishwa na uhodari wa Moyo,kama kuna namna Mungu hajashughulika na moyo wako huwezi kuwa hodari. ✍🏻Mchakato ule ule alioutumia Mungu kuwatoa Israel Misri kwenda Kaanani,anautumia leo katika maisha ya wokovu, unapookoka haufi unabaki Duniani ili ujifunze vita nyingi ushinde. Ufu3:12 Yeye ashindaye... ✍🏻 Mbinguni hatutaingia kwa bonus,ni maamuzi utakayoamua hapa;hakuna maombi na maombezi ya kuingia mbinguni bali ni maamuzi ya maisha unayoishi yataamua uende wapi Mdo10:34-35 Mungu hana upendeleo... ✍🏻Hana heshima za kibinadamu,anashughulika na wanadamu kwa namna alivyowaumba ✍🏻 Hivyo uhodari wa kanisa la mwisho ni uhodari wa jinsi ulivyo hodari kiroho Mithali4:23 Linda sana Moyo wako... Mithal16:1 Maandalio ya moyo... ✍🏻Jukumu la kulinda moyo wako lipo mikononi mwako..Kusema nimejeruhika sana,nimeumia inaonesha udhaifu wako kutotimiza wajibu ✳ a)Eneo muhimu la kutunza moyo wako na kuliangalia ni KIBURI ✍🏻Kiburi ni Roho siyo tabia. Kimezidi tabia,kipo juu ya uwezo wa kibinadamu na kwa juhudi zako huwezi kujitoa. ✍🏻Kiburi huanza kidogo kidogo usiposhughulika nacho kinakua,siyo rahisi kujua kikianza,kikiwa kati na hata kikifika level ya juu kabisa kinakuwa kiburi cha uzima(Hapa haujali lolote,utafanya mambo waziwazi,utaongea,utadhalilisha watu) ✍🏻 Dhambi haiwezi kumfanya Mungu amkatae mwanadamu ila kiburi kilichotangulia dhambi. Rum5:8 Tungali na dhambi Yesu akaja.. ✍🏻Yesu anawapenda wenye dhambi,anachochukia ni ile dhambi ndani yao/wanachofanya; Hivyo kiburi ni hatari kuliko dhambi ✳Dhambi ya Adam na Eva (Baba aliulizwa swali hili na Mungu nini kilisababisha watu hawa kukosea⁉) Mwanz3:1-5 ✍🏻Nini kilimshusha Shetani chini?: Kiburi cha kutaka kufanana na Mungu Ezek28:14-18; Isaya 14:12 ✍🏻 Akaja kuwaangusha wanadamu na kitu kile kile Mwanzo3:5"mtakuwa kama Mungu...*Mwanadamu anakula tunda awe kama Mungu;kama ambavyo Shetani alikataliwa mbinguni ndivyo na mwanadamu akakataliwa Edeni ✍🏻Lucifer alisema nitajiinua,nitapanda,nikae kama Mungu (highest level of pride)kashushwa,Mungu akamkataa. Mwanadamu naye alikuwa akitunzwa Edeni kwa utukufu,akilishwa ila Shetani anakuja na agenda ile ile wakatengwa. ✍🏻 it's true Lucifer alikuwa na utukufu;unaweza ukawa na kiburi cha kitu kama hela,cheo,elimu,uzuri n.k ni kweli unavyo.Neema aliyokuwa nayo hakujua kuchora mpaka kati yake na Mungu ✍🏻Mwanz1:26-27 Tuumbe mtu kwa sura na mfano wetu...ila shetani anawaambia mtakuwa kama Mungu(this is pride) Uende zaidi ya nafasi yako,kama shetani alivyotaka kuwa zaidi ya Mungu. ✍🏻Kiburi ni kibaya pale kuna vitu Mungu ameanzisha ndani yako,kuna neema,kuna mahali kakufikisha kinainuka. ✍🏻 Hivyo kiburi hutangulia uasi;Ilikuwa kwa Shetani na Mwanadamu kabla ya anguko;ukiwa na kiburi dhambi ipo,vinaenda sambamba ✍🏻Zab51:17 Moyo uliopondeka hataudharau..Mungu hajawahi mkataa mwenye dhambi ila mwenye kiburi;kiburi ni hatari kuliko anguko ✳ Njia Rahisi kujipima kama una Kiburi⁉ 1)Wakati unasifiwa:Bila wewe hakuna kinachoweza endelea katika hiyo ofisi,kanisa,kwaya,familia n.k..Unanyanyuka,unainua mabega juu elewa tu una level flani ya kiburi 2)Wakati Unakosolewa:Unajiona upo vizuri wao wanakuona sifuri;unajiona smart,mzuri..angalia unavyoreact;Hata kama wanakukosoa kwa chuki,Yusufu chuki ya ndugu zake ilimsogeza kwenye hatma yake.(Si kila chuki utakuua,nyingine inakupa hatua moja mbele) ✍🏻Jinsi unawachukia watu unawapa hatua mbele kwenye hatma zao..waone wenye dhambi,wachafu...Mungu si mwanadamu ajute Hesa23:19 ✍🏻 Ukilijua hili utaheshimu kila mtu maana anaweza kuwa Nabii wako kesho ✍🏻Unayo stamina unapokosolewa?unasikiliza in positive way na kwenda kurekebisha Mfano:Baba kuanza kufundisha na kiwango cha mafunuo kubadilika alikosolewa na mtu Yako4:6 Mungu huwapinga wenye kiburi... ✍🏻 Ubaya wa kiburi unafunga milango ya kurekebishwa,kusahihishwa,kuwa mtu bora zaidi ✍🏻Yesu hakuna maneno mabaya hakuambiwa(mlafi,mwizi wa mbao,Tapeli,anatoa pepo kwa Belzebul...huyu ni Masihi..wewe leo wanakuchallenge kidogo unasema wananionaje? ✍🏻Jifunze kwa Nebukadreza Dan4:31-33 Alifukuzwa mbali msituni na Mungu ✍🏻 Kuna Aina ya moyo unaweza kukutoa mbugani hadi ikulu kama Daudi; au kukutoa Ikulu hadi mbugani kama Nebukadreza ✍🏻Mungu hatakusikia utaenda maombi yote kama ambavyo akikushusha hakuna wa kukupandisha ✳ Alama za kuonesha una Kiburi 1)Roho ya mashindano ✍🏻Siku zote mwenye kiburi ana mashindano,yeye ndio anastahili ✍🏻 Maisha ni rahisi kama hushindani,unaishi maisha yako na kutenda mapenzi ya Mungu;Shindana nao kuwa na moyo bora ✍🏻Huduma ni Rahisi kama hushindani..mfano Baba yetu hana mashindano na mtu,aliyekuinua na kukubariki na mimi ataniona Mhub9:11 Wakati na bahati humpata kila mtu... ✍🏻Mpongeze aliyefanya vizuri,mfurahie unangoja aharibikiwe ya Nini? *Kuna aina ya uchawi unatembea nao bila kujua(kuchukia wengine wamekupita)*;tumbo linapata moto ✍🏻 Wengi tunapishana na Mungu sababu ya viburi vya moyo;Neema zinatofautiana;Heshimu Neema;katika mwili wa Kristo huwezi kuwa kila kitu;Tunatofautina hatma tusishindane 2)Kujiona Bora kuliko wengine ✍🏻Unaona mpaka wafike bado wanasafari ndefu;unasahau Mungu anaweza kuwapigisha hatua. Mfano Sauli anapojiinua kuna Daudi anaandaliwa porini 1Sam1:16 ..Utamlilia hata lini ikiwa nimemkataa ✍🏻Sauli kwa kiburi afanya kazi ya Kikuhani 1Sam13:8-15 ✍🏻Kiburi kimezuia annointing,Mungu anatamani akusaidie ila kiburi kinamzuia ✍🏻It takes God kusililizwa,kufatiliwa na kuaminiwa na watu,usijione bora kuliko wengine;hakuna mwenye haki ya kuonea wengine; Wengi wapo chini si shetani kawashusha bali ni kiburi Matha12:31 Mpende jirani yako.. 3)Kujihesabia haki hasa unapoonywa na kuchukuliwa hatua ✍🏻Ebr12:6-7 Mwana nimpendaye humrudi.. ✍🏻Makemeo na maonyo ni alama ya upendo ✍🏻Rafiki asiyekuonya huyo ni adui..yeye ni hata mimi..hakuoneshi ujinga na ubaya wako ✍🏻Mheshimu anayekuonya ✍🏻Wengi tumekuwa adui kwa waliotuambia ukweli *Ushuhuda: Baba kufunga siku 100,kufukuzwa kanisani ila alipiga magoti,alilala chini:Kiburi hakikuoneshi kushuka,kuteremka bali kinakuonesha na wewe liamshe,wakati wote utajihesabia haki. ✍🏻Shetani alivyo atakuonesha makosa yao...na maandiko..Watizama boriti..Luk6:41-45 ✍🏻 Kadri hatubebi aibu na utukufu hatubebi;shinda Kiburi,kujihesabia haki SOMO:PART1:UCHAWI NDANI YA FAMILIA NA HUKUMU YA KIUNGU Jpili:Baba kasema tutashughulika na Roho za kichawi ndani ya familia; Ila Hatuji kanisani sababu tuna shida zetu au tunataka kutendewa bali Tunajusanyika kumuabudu Mungu ✍🏻Makusanyiko mengi watu hawamwabudu ila wanataka vitu vya Mungu.Mungu amesema wakinifanyia ibada nikafurahi nitawafungua na kuwasaidia🙌🏿 Mambo 3 ya msingi kuhusu somo hili 1) Kila familia Mungu huinua Kuhani wa kusababisha jina lake litangazwe na liabudiwe kwenye familia hiyo Eze22:30 Nikatafuta mtu.... ✍🏻Yumkini mtu huyo ni wewe unapaswa kuleta heshima ya jina la Bwana Mfano:Ibrahim Baba yake mzee Tera aliabudu Mungu ila Ibrahim akatokea Baba wa imani Yosh24:2 ✍🏻Kila familia yupo mtu anayesimama kama Kuhani ili heshima ya Mungu iletwe;It's a spiritual principle,huwezi kuzaa watoto wote ukakosa Daudi 2)Kila familia shetani huinua Kuhani wa kusababisha jina lake litajwe na kuabudiwa ✍🏻It may take time but it's a satan strategy ✍🏻Utajuaje kuhani huyo⁉Anahangaika kwa waganga,anapenda uchawi,usidhani anashughulika na maisha yake tu..ni kuhani (mme,mke,mjomba,shangazi n.k) ✍🏻Mnaomba huku yeye anaomba kwa miungu ✍🏻 Huwezi kusema mimi ni Mkristo wakati unalala kwa waganga,makaburini na Yesu alishatoka makaburini yupo hai ✍🏻Huyo amesimamishwa kwenye hiyo familia kama kuhani wa giza ✍🏻Kama umeokoka peke yako wewe ni Kuhani wa kuleta majibu na kumtambulisha Mungu kwenye hiyo familia 3)Vita ya kiroho ni vita kali kwa watu wengi kwa sababu ya nafasi ya Kikuhani katika familia ✍🏻Wengi wameacha wokovu kwa kishindwa kusimama katika nafasi ya Kikuhani,vita ikawa nzito..hawa wanataka kutawala kwa giza wewe unaleta maombi bila maarifa..wanakuinukia ✍🏻Watu wengi wapo katika vita ya Kikuhani katika familia na maagent wengine ni ndugu zao wanaokula nao pamoja ila hawajui ✍🏻 Good news is Daudi alimuua Goliath; Ester alining'iniza kichwa cha Hamani;Yesu at 33yrs old aliokoa ulimwengu wote🙌🏿 ✍🏻Yosh24:15 ina maana kiti cha familia na ukoo anayetawala ni Bwana mwenyewe ✍🏻Mdo10:44-48 Kornelio na nyumba nzima wakamwamini Mungu;kiti cha ukoo alikalia Mungu ✍🏻 Picha hii ilimtesa mwanzilishi wa Taifa la Israel mzee Yakobo 👉🏻Anakutana na mfumo wa kishetani kwa Labani 👉🏻Akampenda Raheli mbeba uchawi wa babaake Mwanz31:19 👉🏻Yakobo ana agano na Mungu 👉🏻Mungu akamtokea Laban asimdhuru Yakobo Mwanz31:24 👉🏻Wakaweka agano la mauti Mwanz31:43-55..aliyekuwa na uchawi ukamfaidisha hataacha ✍🏻 Yakobo aliyekutana na malaika wa kutosha hakujua kama Raheli ana vinyago vya babake;sijui kwa namna gani wewe upo salama na hiyo familia yako ✍🏻Kuhani wa giza huwa wanahukumiwa na Mungu..Raheli alikufa ili Hesab23:23 isimame ✍🏻Suleiman na neema yote uchawi ulimgeuza moyo 1falme11:1-25 Baba amesisitiza tusikose muendelezo wa somo hili muhimu litatufumbua macho

Comments

No comments yet.

Please login to comment.