cover

DAY 8 : EL RACHUM

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church • 2025-09-09
ScripturesMwanzo 20:5-6

*Na Ev Daniely Joshuan*_ *08th September 2025* *HATUA ZA KUUANDAA MOYO ILI KUZIPATA REHEMA ZA MUNGU KWENYE MSAMAHA* *HATUA YA TANO* _*KUANZA KUPOKEA NA KUFURAHIA MAONYO YA KIMUNGU.*_ Moyo wa Mwanadamu ukiharibika mwanadamu anakataa maonyo ya Mungu. Naomba nikuanbia mambo machache ya muhimu. Mbingu ufungua maonyo ili kufungua rehema zake. Sijajua kwamba unajua Mungu anapokuonya maana yake anataka kuachilia rehema zake kwako. Mungu anapokuonya anatarajia utubu wala si kuasi. Ukiona Mungu hakuonya jua kwamba amekutupa siku nyingi anasubiria eneo la kukumaliza tu. Yona alijua kwamba Mungu anavyowaonya watu ni watu anaowapenda. Yona alijua kwamba maonyo yale yalikuwa yanahitaji watu waombe rehema. MTU MUNGU ASIYEMUONYA NI MTU ASIYEMJUA AU NI MTU ASIYE NA MPANGO NAYE. *Mungu uwaonya watu anaowajua, Mungu uwaonya watu alio na mpango nao.* Mungu akikutuma kuonya mtu kuwa makini jua kwamba Mungu anampenda ndiyo maana anamuonya nenda taratibu. Mungu hawezi kuonya mtu asiye na mpango na yeye. Kama Mungu akiwa na mpango na wewe atakuja mpaka kwenye ndoto zako. Kuna watu ambao usingizi kwao pia ni mateso kwasababu unapambana na Mungu. Ndoto ni tamu na nzuri kama unatembea vizuri na Mungu. Abimeleki alionywa na Mungu kwenye ndoto kwa ukali. Ingawa unaweza kuona kama vile hakukosea nilishakuambia haki ya mwanadamu si haki ya Mungu. *Mwanzo 20:3-6* _*[3]Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu. [4]Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki? [5]Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi. [6]Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.*_ Mungu akikuonya anakujua rafiki yangu. Ndiyo maana madhabahu ya kweli imejaa maonyo. *Zaburi 141:5* _*Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.*_ Mungu uwaheshimu watu ambao wanakubali maonyo. *HATUA YA SITA* _*ANZA TENA KUYAPOKEA MAAGIZO YA BWANA.,*_ Kabla ya watu kukosea mioyo yao utii maagizo. Ishara ya kwamba moyo wako umeharibika ni vile ambavyo unatii maelekezo. *Mithali 4:13* _*Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako. Take fast hold of instruction; let her not go: keep her; for she is thy life.*_ Andiko ili tumezoea kulisema mshike sana elimu lakini andiko ili ukisoma kwa kiingereza linaongelea swala la kukamata maagizo. Moyo ulio karibu sana na maagizo ya Mungu uko karibu na rehema za Mungu. Siri ya maagizo ya Kimungu ni kwamba Mungu anapoendelea kukuagiza ana mpango na wewe. Mungu anapokuangiza maana yake hajatengeneza copy yako. Mungu ana nakala ambazo wewe ukiziona utaona namna ambavyo ulikuwa mjinga katika yale uliyotenda. *Ezra 10:11* _*Sasa basi, ungameni mbele za BWANA, Mungu wa baba zenu, mkatende alipendalo; mkajitenge na watu wa nchi, tena na wanawake wageni.*_ *Isaya 56:1* _*BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.*_ *Mithali 20:9* _*Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?*_ *Mithali 22:11* _*Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake.*_ *Restoration Gospel Commission Ministry,* *P.O.Box 32520,* *Goba Centre, Dar es salaam, Tanzania,* *Email: info@rgcm.org,* *Contact: +255 764 711 544,* *Web: https://www.rgcm.org.*

Comments

No comments yet.

Please login to comment.