DAY 7 : EL RACHUM
ScripturesYeremia 17:5
*Na Ev Daniely Joshuan*_
*07th September 2025*
*HATUA ZA KUUANDAA MOYO ILI KUZIPATA REHEMA ZA MUNGU KWENYE MSAMAHA*
UTAUANDAJE MOYO WAKO ILI UZIOATE REHEMA ZA MUNGU?
*HATUA YA NNE*
_*ANZA KUMTUMAINI MUNGU KWA UPYA KWA MOYO WAKO*_
Moyo uliorudisha matumaini kwa Mungu uko karibu sana na rehema za Mungu. Moyo wa mtu ukigeuza uwa unageuza na matumaini ya mtu. Kuna watu mioyo yao ilivyogeuzwa wakaanza kutumaini wanadamu.
Ni kitu cha hatari sana kuwatumaini wanadamu. Utajua hawako upande wako siku ambayo kuna mahali utapita. Biblia inasema *Yeremia 17:5* _*BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.*_ Wanadamu uwa wanafutika na wanadamu wanakufa ndiyo maana Biblia inasema *Mithali 3:5* _*Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;*_. Inawezekana moyo umegeuka na ukaanza kutumaini fedha pia. Sasa unapoanza kutafuta rehema za Mungu lazima uanze kuyasahau matumaini bandia.
Kuna watu wakati walipokuwa hawana fedha walimtumaini Mungu. Inawezekana ni fedha ulizonazo ambazo zinakefanya usimtafute Mungu. Hakuna mtu anazifikia rehema za Mungu kama matumaini yake hayopo kwa Mungu. Kuna watu inawezekana ni cheo ndicho anakitumainia. Matumaini bandia yanawezekana ni nafasi uliyonayo. Wengine wanasababu kwamba mbona ni kitu cha kawaida cha kutumia akili tu. Watu hawaoni sababu ya kutubu kwasababu matumaini yao yameelekezwa kwenye akili walizonazo.
Wako watu ambao wameshindwa kuzipata rehema za Mungu kwasababu ya matumaini bandia waliyonayo.
*Zaburi 32:10*
_*Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka. Many sorrows shall be to the wicked: but he that trusteth in the LORD, mercy shall compass him about.*_
Tumaini lolote bandia linakufukuzia rehema za Mungu. Ndiyo maana Mungu wakati mwingine ili hawapate wanadamu eneo la rehema anapukutisha vitu vyote. Kama ambavyo ilikuwa kwa Nebukadreza. Kila mtu anayemwamini Mungu na kumtumainia Rehema zitamzunguka.
Ikiwa umeondoa matumaini kwa Mungu umeziondoa rehema za Mungu. Je unamtumaini Mungu au kazi uliyonayo? Unamtumaini Mungu au watu ulionao, cheo ulichonacho, fedha ulizonazo? Watu wengi wameondolewa kwenye kiwango cha rehema kwasababu ya matumaini bandia waliyonayo.
Kuna wakati unasimama mwenyewe mbele za Mungu unasahau watu waliokuzunguka, unasimama mbele za Mungu na unasahau cheo ulichonacho.
Nebukadreza alijitia ubabe akaona cheo alichonacho majeshi aliyonayo. Sijui siku ukisimama mwenyewe nani atasimama pamoja na wewe kama Mungu hatakuwa upande wako. Rehema zitakuzunguka ikiwa tu utamtumaini Bwana.
*Restoration Gospel Commission Ministry,*
*P.O.Box 32520,*
*Goba Centre, Dar es salaam, Tanzania,*
*Email: info@rgcm.org,*
*Contact: +255 764 711 544,*
*Web: https://www.rgcm.org.*