cover

DAY 6 : EL RACHUM

Ev Daniel • RGCM-GOBA • Apostolic Church • 2025-09-06
ScripturesMithali 4:4

*Na Ev Daniely Joshuan*_ *06th September 2025* *HATUA ZA KUUANDAA MOYO ILI KUZIPATA REHEMA ZA MUNGU KWENYE MSAMAHA* *HATUA YA TATU* _*ANZA KURUDISHA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO*_ Hii ni hatua muhimu sana. Rehema za Mungu zitakurudia wewe rafiki yangu pale ambapo utaanza kurudisha neno la Mungu kwenye maisha yako. Nafikiri unajua kwamba Mtu akimkosea Mungu neno la Mungu linakuwa siyo la muhimu tena. Shetani ni mbaya kwasababu uipa neno la Mungu ndani ya wanadamu. Ukianza kuona muunganiko wa neno umeanza kutiririka ndani yako maana yake uko karibu na Mungu. Kuna watu wanajua kwamba walikuwa karibu na Mungu kwa kusoma neno na walikuwa wanasikia raha kusoma na walikuwa wanaelewa. Lakini sasa hivi hawaelewi neno kabisa. Hatua hii ni ya muhimu ya kuanza kurudisha neno na ni maamuzi binafsi. Daudi katika Zaburi yake ya 51 moja ya kitu anasema *Zaburi 51:13* _*Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.*_ Maana yake anajiba wajibu. Ikiwa kwenye kukosea kwako hakuna mtu ambaye amejifunza ujue kwamba hiyo shida bado itakurudia. *Mithali 4:4, _*Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.*_ *Luka 4:4* _*Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.*_ Maisha yetu yamefungamanishwa katika neno la Mungu. Na leo nataka kusisitiza zile hatua za usomaji wa neno. Kuna watu wanasoma Biblia ili kutafuta ufunuo ili wakasisitize wengine. Hakuna msomaji yeyote wa Biblia anayemsomea mwingine kabla ya kujisomea mwenyewe. Huo ni moyo wa uasi na uko kinyume na mamlaka ya neno. Mamlaka ya neno lazima ikunyenyekeshe wewe kwanza kabla ya mtu mwingine. Soma neno kwaajili yako kwanza, usiwaone watu wengine kwenye maandiko jione kwanza wewe. Lifanye neno kwaajiki yako kwanza. Nimeandika hatua tano za usomaji wa neno kwenye kitabu changu cha waogofu wapya na leo nataka kuongeza hatua ya sita. *Hatua ya Kwanza* _*Lazima ufanye maandalizi ya kusoma neno.*_ Tenga muda Mungu hatakupa muda alishakupa pumzi. Huu unafiki wa kumuambia Mungu naomba muda hatakupa muda. Tenga muda wa kusoma neno la Mungu. Wewe ni mfu kama hausomi neno la Mungu. _*Tafuta Biblia*_ Nunua Biblia kabisa na muonyeshe Mungu uko serious. Usitumie Biblia ya kwenye simu maana ina mambo mengi bado. Sijui kama umekomaa kiasi cha kusoma Biblia kwenye simu na ikaingia fedha kwenye simu na ukaendelea kusoma neno bila kuangalia. Wako wapi watu ambao leo wanaenda na Biblia ibadani. Yesu mwenyewe alipoingia hekaluni alichukua chuo cha gombo. Acha uzungu usio kuwa wa kawaida. Kwenye maandalizi hayo hayo andaa maandalizi ya kusoma neno. Andaa mazingira kuna watu ambao wanasoma Biblia wakiwa wanakunywa uji. *Hatua ya Pili* _*Amka Soma*_ Tulia ili uweze kuelewa kile ambacho unasoma. Watu wanaweza kuwa na Biblia na wasielewe. Yuke mtu wa Ethiopia alikuwa na chapisho kutoka Hekaluni lakini hakuwa anaelewa. Huyu Toashi angewafundisha nini watu ambao walikuwa Kushi kipindi kile kama Mungu asingeingilia kati wakati anasoma chuo cha Nabii Isaya. Soma neno maana neno la Mungu li juu ya changamoto zote unazopitia, mateso yote unayopitia . *Hatua ya Tatu* _*Kutafakari Neno la Mungu.*_ Usisome neno la Mungu kama mshabiki tafakari. *Yoshua 1:8* _*Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.*_ Watu ambao ni washindi ni wale ambao wanatafakari neno la Mungu si changamoto walizonazo. *Mathayo 7:24* _*Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;*_ *Hatua ya Nne* _*Kuliishi Neno la Mungu*_ Tafuta neno ambalo linahusiana na changamoto unayopitia. Hakuna tatizo jipya kwenye maisha ya mwanadamu wewe tafuta neno la Mungu na simamia. Watu wana mapito magumu lakini yote yameandikwa kwenye Biblia. Kataa maneno yote uliyoambiwa yaliyo kinyume. Kumbuka kwamba maisha yanaamriwa rohoni si na maneno ya watu bali nen9 la Mungu. Tunaishi sawa na neno linavyosema si marafiki au watu wanavyosema. Litii neno maana neno halijawahi kumuangusha mtu. Neno litasimama vyote vitapita. *Hatua ya Tano* _*Kuwashirikisha wengine*_ Neno lolote ambalo unasema umelielewa na hauwashirikishi wengine ilo neno ujue haujaelewa. Nitakufundisha hatua nyingine wakati mwingine. *Restoration Gospel Commission Ministry,* *P.O.Box 32520,* *Goba Centre, Dar es salaam, Tanzania,* *Email: info@rgcm.org,* *Contact: +255 764 711 544,* *Web: https://www.rgcm.org.*

Comments

No comments yet.

Please login to comment.