DAY 2 : EL RACHUM
Scriptures*Maombolezo 5:21*
*03rd September 2025*
Wakati mwingine utajua namna watu mioyo yao imeharibika kwa namna wanavyoongea. Ukiona mtu anasema mabaya juu ya ndoa, huduma yake au chochote ambacho Mungu amemuhusicha kwacho ujue moyo wake umeharibika. Moyo unaweza kuharibiwa kwa uchungu au hasira kama wakati ule wa Kaini. Kaini anamwambia Mungu *Mwanzo 4:9* _*Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?*_
Majibu hayo alikuwa hampi mwanadamu wala Mchungaji wake bali Mungu aliyeziumba mbingu na Nchi. Utaona namna ambavyo moyo wa mwanadamu ukiharibika unavyokuwa. Hivyo hivyo utaona kwenye kanisa la kwanza la Mitume kwa mtu alikuwa anaitwa Anania na Safira.
*Matendo ya Mitume 5:3-8*
_*[3]Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja [4]Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. [5]Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. [6]Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika [7]Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. [8]Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.*_
Moyo ukiharibika unaweza kuona namna ambavyo watu wanaweza kusema uongo. Unaweza kusema hawakupata nafasi ya toba lakini Mungu aliwapa nafasi ya kutubu ndiyo maana Petro aliuliza.
Moyo wa mwanadamu unaweza kuharibiwa na vitu vingi si dhambi pekee. Unaweza kuwa mtakatifu lakini maneno yakaharibu moyo.
* Dhambi inaharibu moyo.
* Maneno
* Chuki
* Hasira.
Kuna watu ambao wanafanya vitu lakini mioyo yao haipendi. Watu wanafanya zinaa lakini mioyo yao haipendi. Ndipo hapo utakutana na mtu kwa namna anavyoongea unajua moyo wake umeharibika.
*Faida ya kuwa na moyo ambao haujageuka ni ukaribu na rehema za Mungu.*
Ukiona moyo wako unegeuka una kazi ya kufanya. Hakuna namna ambavyo Mungu anaweza kutembea na watu nje ya mioyo yao. Ndiyo maana anasema Tazama nasimama mlangoni nabisha hodi ufunugue. Moyo wako ukigeuzwa ukawa mgumu ukawa wa jiwe moja kwa moja unakuwa mbali na yeye.
Ngoja nikuonyesha mfano wa wanafunzi wa Yesu kati ya Petro na Yuda. Petro alikuwa anafanya makosa mengi tofauti na Yuda, alikemewa mpaka akaambiwa rudi nyuma yangu shetani. Lakini Petro huyo ndiye ambaye Bwana alimwachia kanisa. Petro alikuwa karibu na rehema za Mungu.
Yuda tangu siku ya kwanza moyo wake ulikuwa mgumu. Yuda alimtesa Yeus kwenye huduma alikuwa anaiba sadaka. Yuda alikuwa mfano wa mtu ambaye Moyo wake ulikuwa mgumu. Na baada ya yale yote utaona namna ambavyo Yuda alikwenda na kujiua. Hakuna mtu ambaye ana moyo mgumu atakayemaliza salama kama asipogeuka.
Watu wana maisha mabaya kwasababu ya mioyo mibaya. Asilimia kubwa ya watu ambao wana mioyo mibaya wana maisha mabaya. Ukiwa na moyo mbaya maana yake unakosa usaidizi wa Kimungu. Utakuwa na bidii kubwa lakini utashangaa unakuwa na ugumu ambao haujui umetoka wapi.
Kuna watu wanapita mahali pagumu kwasababu wana mioyo migumu. Jiulize ungekuwepo kipindi cha Nebukadreza namna ambavyo alipelekwa porini kwa vipindi saba. Kama ungekutana na Nebukadreza ungemsaidia namna gani? .
Hadhari za mioyo migumu hautamaliza vizuri, kama ni kazi hautamaliza vizuri. Lazima ukubali Mungu haufinyange moyo wako na kuutengeneza vizuri. Biblia inasema heri wenye moyo safi maana wao watamuona Mungu. Watamuona namna gani? Wakiwa kwenye kazi za mikoni yao watamuona Mungu, wakiwa ofisini watamuona Mungu.
Unaweza kumfanyia mabaya na kufanya chochote unachoweza kufanya lakini kwasababu ni mwenye haki hayatampata mabaya. Ni kwa wabaya pekee mabaya uwapata.
*Zaburi 1:6*
_*Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.*_
Ukiweza kuutunza moyo wako maana yake uneweza kumtunza Mungu. Mungu aliniambia Ukitaka kutofautiana na watumishi tofautiana nao moyo. Chagua kuwa na moyo safi, unapokuwa na moyo safi maana yake umeruhusu rehema za Mungu kwenye maisha yako.
Biblia inasema *Mithali 4:23 * _*Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.*_
(Mfano wa Pili ni Anania na Safira.*
Unaposiki habari za wakins Petro ni watu ambao walikuwa na nguvu kupita kawaida. Na wakina Anania na Safira pamoja na kuwa katikati ya wachungaji wa namna hiyo lakini mioyo yao ilikuwa imeharibika.
*Mfano wa Tatu ni Farao*
Farao alikuwa mtu mwenye kiburi kwa wakati ule. Farao alikuwa amejaa kiburi saa unamuona mtu kama huyo anazama usije kumpa msaada utanunua ugomvi na Mungu. Farao alikuwa na moyo mgumu na aliwafuta Waisraeli mapaka kwenye bahari ya ya Shamu.
Moyo mgumu ukiwa ndani yako Mungu anaweza kukuzika baharini na utajuaje kwenye maisha yako kuna makosa makubwa ulifanya. Kama uliwahi kuolewa au kuoa utakundua kuna kitu hakikuwa sawa. Kama ulikuwa na huduma kubwa utagundua iliwahi kupigwa ukaanza moja. Hii ni tafsiri ya wazi kwambauna moyo mgumu. Na unaweza kuwa na moyo mgumu lakini una moyo mgumu.
*Mfano wa Nne ni watoto wa Eli*
Hawa wote ninaokuambia utaona mwisho wao haukuwa mwema. Kipinfi kike wana wa Eli walikabidhiwa madhabahu walifanya walivyokuwa wanataka. Walikuwa kwenye hekalu la Mungu lakini walikuwa wanafanya mabaya mbele za Bwana. Wana wa Eli hata walipoitwa na Baba yao kuwauliza wala hawakusikiliza na Biblia inasema kwasababu Mungu alikusudia kuwaua. Na mwisho wake walikufa.
*Mfano wa Tano mtoto wa Yuda*
Mwanzo 38:7
_*Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua. And Er, Judah's firstborn, was wicked in the sight of the LORD; and the LORD slew him.*_
Eri alikuwa mbaya na unaposoma Biblia ya kiingereza utaona ikisema alikuwa mwovu na Mungu alimuua. Na utaona mtoto mwingine wa Yuda kwenye mlango wa 38.
*Mwanzo 38:8-10*
_*[8]Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. [9]Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. [10]Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye naye.*_
Ukitaka kuzifikia rehema za Mungu kwenye maisha yako lazima uhakikishe una moyo ambao haujagezwa au haujageuka.
*Mungu huzuia kwa hasirq rehema zake kwa wati wote wenye mioyo mibovu*
Moyo wako ukikaa karibu na Mungu vitu vingi vitakaa karibu na wewe. Kila ulichonacho kitakuwa kari na wewe. Mungu huzuia kwa hasira rehema kwa watu wenye mioyo miovu na hapa ndipo kuna kazi kubwa.
*Zaburi 77:9*
_*Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?*_
*Zaburi 77:9-20*
_*[9]Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake? [10]Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.[11]Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. [12]Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. [13]Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?[14]Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. [15]Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu. [16]Ee Mungu, yale maji yalikuona, Yale maji yalikuona, yakaogopa. Vilindi vya maji navyo vikatetemeka, [17]Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa. [18]Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika; [19]Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.[20]Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.*_
Huyu ni mtu ambaye alikuwa anatafuta rehema za Mungu. Mungu kuzuia kwa hasira rehema zake kitendo hicho anataka urudi kwenye fikira zako mwenyewe na ujue ya kwamba bila yeye hauwezi kwenda alafu kubali kuvunjia kwa yeye mwenyewe sirini. Shuka mpaka mavumbini na utaona namna ambavyo Bwana anarejesha rehema zake.
*Maombolezo 5:21*
_*Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.*_
Uhamsho umekuja kwaajili ya mtu mmoja na haijalishi uko wapi au kwenye hali gani Mungu anakuita.
Nimewahi kuimba vizuri watu wakabarikiwa lakini nikawa na moyo wa jiwe hivyi nikabaki mtupu nina jina lakini sina milango nina jina lakini sina kibali, nina jina lakini sina utukufu wako. Nimewahi kuhubiri mataifa na mataifa nina jina lakini milango imefungwa. Nimeachwa maisha yangu ni ukiwa familia yangu ni ukiwa. Nakumbuka nyakati zile nikienda mkoa kwa mkoa kuhubiri habari zako lakini leo nimerejea kwenye ulevi.
Mungu amelituma neno lake ili ujue kwamba majira ya kukaa porini yanatosha sasa.
*Restoration Gospel Commission Ministry,*
*P.O.Box 32520,*
*Goba Centre, Dar es salaam, Tanzania,*
*Email: info@rgcm.org,*
*Contact: +255 764 711 544,*
*Web: https://www.rgcm.org.*