Wito wa Mahali pa siri - Day 1
ScripturesMathayo 25:33,Zaburi 91:1-2
WORD OF GOD Mathayo 25:33
HEAD OF THE SUBJECT : WITO WA MAHALI PA SIRI
TUTOR : HOLY SPIRIT
PREACHER : EV. Daniel
LOCATION : RGCM - GOBA
DATE : 21st Nov 2023
Shalom Baba na Kuhani wetu!Tunamshukuru Mungu kwa kuruhusu maarifa haya ili tusitembee katika makosa🙏🏿🙌🏿
PART1:THE CALLING TO THE SECRET PLACE/WITO WA MAHALI PA SIRI
✍🏻 Ni somo la kimaelekezo
✍🏻 Kuna watu hawajui na wakishajifunza wataamua kukaa mahali pa siri
✍🏻 Kuna watu waliokuwa wamekimbia/wameondoka mahali pa siri;baada ya somo watagundua walikuwa wameondoka pahali pa siri
MAMBO MUHIMU YA KUJUA
1)Kama hutajua mahali pa siri hautakuwa katika kina cha imani
✍🏻Kama hutaamua kukaa/to dwell mahali pa siri utakuwa mkristo wa kawaida,mtu wa dini,huwezi kuwa mtumishi mwenye kina,mwanamaombi n.k maana hujui kukaa mahali pa siri.
✍🏻Wakristo wengi hawana maarifa juu ya mahali pa siri hivyo wamekuwa wa kawaida;huwezi kuwa na kina katika maisha ya kiroho au ya kihuduna kama hujui kukaa katika mahali pa siri
2)Mungu anaguswa sana na watu wanaokaa katika mahali pa siri
✍🏻Hufurahishwa;Anawatafuta waabuduo katika Roho Yoh4:23; ina maana hawapatikani kirahisi;nyakati hizo ndio hizi sasa
3) Usipojua kukaa mahali pa siri unakuwa Mkristo wa kawaida
✍🏻Unaweza kuzaliwa kanisani ila Yesu hajazaliwa moyoni mwako;ni muhimu sana Yesu azaliwe moyoni
✍🏻Ukristo ni uhusiano na ukaribu na Mungu na siyo dini.Tuna Wakristo wengi ambao ni watu wa dini tu.
👉🏻 Utajuaje wewe ni mtu wa dini⁉
i)umezaliwa kanisani ila Yesu hajazaliwa moyoni
ii)Unahudhuria kanisani ila tabia zako hazibadiliki;watu wa dini ibada ni muhimu kuliko uhusiano wao na Mungu
-Yesu alisema enendeni mkawafanye kuwa wanafunzi..Matha28:19
*-Yesu alianzisha kanisa ili watu wabadilike
iii)Wanajitahidi kufurahisha watu kwa kiwango kikubwa na si Mungu
4) Nje ya kuketi mahali pa siri hakuna thawabu yoyote utakayopata kutoka kwa Mungu
✍🏻Wanaomba,wanatoa ila hawaoni matokeo
✍🏻Wakati wa Yesu alitoa thawabu si kwa watu wa dini
✍🏻Mungu ameutengeneza Ufalme wake na thawabu
Mithal22:4
✍🏻Utakuwa mtumishi mzuri usiye na thawabu;kuna watu wamemchagua Mungu ila hawana thawabu,wanajua taratibu za kanisa ila hawana thawabu
✍🏻Thawabu inatofautisha kati ya kanisa A na B,Mchungaji A na B
✍🏻Utafunga hata ubaki mifupa hutaona matokeo,utamuona Mungu mbaya.
✍🏻Fedha hainunui thawabu
✍🏻Maisha,huduma ni nyepesi sana kama unajua kukaa mahali pa siri
Ushuhuda:Kijana mpiga kinanda kanisani..
5)Mahali pa siri si mahali pa kimwili bali ni mahali pa kiroho
✍🏻Unaweza ukawa muhudhuriaji mzuri wa ibada ila hujakaa mahali pa siri
6)Mungu wetu anaketi sirini na anaona sirini
✍🏻Matha6:18 :kuna sifa mbili za Mungu hapa;Kukaa sirini & Kuona sirini
✍🏻Mungu hatiishwi na wanaoenda kanisani;wanaoenda kanisani ni wadini na hawabadiliki maisha yao.
Matha23:27 Wanapaka chokaa makaburi..
✍🏻Dini inahangaika na nje tu ila wana sifa kubwa ya watenda dhambi waaminifu
7)Kuingia mahali pa siri ni gharama mno ingawa kutoka ni rahisi tu
8)Mahali pa siri ni mahali pa ulinzi,Pendo na shibe
✍🏻Baada ya anguko mwanadamu walitolewa mahali pa siri
9)Tunakutana na Mungu mahali pa siri na si barabarani
✍🏻Mafundisho,unabii,directions za kiroho,directions za maisha zinapatikana mahali pa siri
✍🏻 Nje ya mahali pa siri ni maisha ya hofu;Perfect sinners
Yoh8:1-11
i)Unaficha dhambi
Verse9(walikosa siku zote hichi;kushtakiwa dhamiri zao)
*-Unaona dhambi ya mwingine kumbe na wewe ndiyo unaitenda hiyohiyo
ii)Hufahamu dhambi yako
*-Una kiburi hujui
*-Daudi akamwambia Bwana unichunguze
-1Yoh1:8 Tukisema hatuna dhambi..
👉🏻 Kadri unamkaribia Mungu unajua udhaifu wako
👉🏻Neema inatupa kusimama
👉🏻Damu ya Yesu inatofautisha mmataifa na mtenda dhambi aliye ndani ya kanisa
Efes4: Aliwatoa wengine... Mchungaji asiyekukamilisha,asiyekwambia ukweli ataingia jehanamu kwa dhambi yake na yako
Matha25:33 atabagua kondoo na mbuzi
✍🏻 Kwa nini upo hai?Mungu anakupa nafasi kurekebisha Ufu3:2
Zab84:10
Nini Maana ya Mahali pa siri⁉
i)Ni mahali pa uhalisia wako na Mungu
*-Moyo wa mwanadamu unakutana na Moyo wa Mungu
ii)Mahali moyo wa mwanadamu hushibishwa
iii)Mahali pa uwepo wa Mungu
-Daudi akasema usinitenge na uso wako Zab51:11
-Kuto33:15
iv)Mwanadamu anakutana na Mungu na moyo wa Mungu unafurahi
*-huyatafuti yako bali yatokayo katika Moyo wa Mungu
*-uso wa Mungu ukafurahi
Mf Ibrahim alimfurahisha Mungu
Nehe8:10
v)Mahali tunaweza kumsikia Mungu
vi)Si mahali pa kimwili bali ni sehemu ya Mungu ndani yetu
vii)Mahali ambapo si kwaajili ya watu maalumu bali ni kwa kila mmoja aliye tayari
Mf:Baba yetu Mafundisho anayotupatia mwaka mzima yanatoka mahali pa siri(anajua gharama)
viii)Mahali ambapo utajazwa amani,furaha na upendo
*-hautapata hivi nje ya mahali pa siri
Matha11:28- tumeokolewa tuwe na furaha
Fili4:4
Uf5:9-10
*-Shetani anapotaka kuharibu maisha yako anaharibu amani
*-Tunza amani yako
*-Anaitwa Shalom
10)Kaa na Mungu vizuri ingia naye sirini atakupa ndoa ya furaha,huduma ya furaha na watu wa furaha
11)Safari ya kuelekea mahali pa siri si nyepesi ila thawabu na matokeo yake hayapimiki wala kuelezeka
12)Safari hii itakutaka kumtafuta Mungu kwa moyo wako wote,kumsogelea yeye na kumtaka kweli kama Mungu wako
13)Kupajua na kupaendea mahali pa siri ni safari ya imani na mahusiano
14)Mahali pa siri ni mahali ambapo ukiondolewa unahisi upo mbali na Mungu na ukishazoea hali ya kuwa mbali na Mungu unakuwa mtu wa dini
*-Utafanya vitu kwa experience
*-you have disconnected
15)Unaona kwa makosa haya Mungu hakupokei
*-Mungu alimtafuta mwanadamu baada ya anguko Edeni
*-Haijalishi ulikosa nini unaweza kurudi mahali pa siri
16)Kufika mahali pa siri unahitaji mambo matatu
a) Muda
b) Bidii ipitayo kawaida
c) Kujitoa kupita maelezo
✍🏻 Baba na Kuhani wetu amesisitiza tusikose muendelezo wa somo hili siku ya ijumaa sa kumi ambapo atafundisha Namna ya kupaingia mahali pa siri;Faida za mahali pa siri na Namna ya kushinda vizuizi vinavyotuzuia kupaingia mahali pa siri.
Daddy I honor the grace of God upon you and upon the Altar🙏🏿🙌🏿